Wednesday, September 7, 2011

Huku na kule kule na huku

Wahaya wana msemo wao kuwa ngombe hali nyasi zilizoko karibu na kwao au zizi, msemo huu pia upo kwa kiingereza kuwa, the grass is always greener outside the gate. Ndivyo ilivyo kwa maisha ya binadamu nah ii ndiyo hufanya maisha na hujenga uchumi na mishughulisho ya maisha ya kila siku.

Najiangalia nisafiripo, kila mara natoka upande mmoja kwenda mwingine, wakati naelekea kule, kuna watokao kule kuja huku, wengine hushukia njiani na wengine hawanasafari japo kuna siku watasafiri tu. Hii ndio hujenga nakuleteleza biashara adhim ya usafirishaji, mradi maisha yaenda. Na nikweli ng'ombe hali majani ya karibu kwani ni vigumu kumuona mmiliki wa basi ulisafirialo akisafiri kwa basi hilo. Mara nyingi kwa ubize na uharaka labda na kile kiitwacho 'hadhi' yake, atasafiri kwa ndege kama sio kwa gari binafsi.

Ni maisha, kuna waafrika watamanio kuishi ulaya japo pia kuna wazungu kibao ambao Africa ndo poa kabisa kwa maisha na ulaya hakufai. Hii huchanganya tamaduni maisha na mienendo. Kuna wabadilishao dini na kuzipondo zile za zamani na waletao mpya pia. Kuna wazarauo tamaduni za kwao au zawengine.


 

Ni huku na kule, kule na huku na labda ndo maisha yenyewe. Lakini ushawahi kujiuliza ingekuwaje kama sote tungekuwa na hitaji moja kwa wakati mmoja? Yaani ingekuwaje kama sote tungeelekea sehemu moja kwa wakati mmoja na labda wakati wote? Anagalia jiji la Dar lilivyofurika na angalia foleni za kutisha mida ya asubuhi na jioni nah ii sio kwamba wakazi wote wa Dar wanaelekea Mijini asubuhi na makwao jioni bali ni kwamba ni wengi wao tu na sio wote, inekuwaje wote?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Sijui kwa nini isiwe huku tu na na sio kule? Nimeipenda mada hii na kuna kitu nimekipata...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ukweli ni kwamba kama binadamu hatujui tukitakacho na kila siku ni mihangaiko ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya kubahatisha tu. Ati, ni nani ana uhakika na akifanyacho katika dakika hii? Ni kweli ndicho unachopaswa kuwa unakifanya katika wakati huu? Ni lazima kweli uende mjini wakati huu? Ni lazima uendeshe gari lako badala ya kupanda daladala? Ni lazima kweli uishi Marekani/Ulaya/Bukoba?

Wengine watakwambia kwamba kutojua huku pengine ndiko kunakoyafanya maisha yaishike na yasiwe mkururo wa matuko ya kawaida yanayosinya (sinya - boring). Maisha!

Mimi ningependa sana kama tungekuwa na uwezo wa kuwa katika sehemu mbili au zaidi kwa wakati mmoja. Ningependa sana kuwa Usukumani na wakati huo huo nikawa Marekani au Bukoba kwa Kamala. Nimefurahi kusikia wanafizikia wakisema kwamba pengine siku za usoni hili litawezekana kama mahesabu yao mapya yako sahihi.

Mada nzuri na yenye kufikirisha sana!!!