Thursday, October 27, 2011

eti kwanini mambo ya pound ya uingereza iko juu kuliko USD? angalia majadiliano na bwa mdogo hapo

Uingereza wana Gold reserves nyingi kuliko US ndio maana thamani yao bado iko juu, hata ukicheki Gold Dinnar ya Libya hapa bongo ina thamani kubwa kuliko Dola ya marekani
Emmanuel Joatham Kamala: Dinari moja ni karibia sh. 4000 hivi

[5:23:50 PM] Kamala J lutatinisibwa: kumbe kijana????

[5:24:01 PM] Emmanuel Joatham Kamala: yap yap

[5:24:20 PM] Kamala J lutatinisibwa: sikujua, then sisi tuna gold nyingi lakini tunazidi kuwa masikini tu na shilingi inaporomoka

[5:26:26 PM] Emmanuel Joatham Kamala: Dollar ziko nyingi kwenye mzunguko sababu ya organisation moja inaitwa federal reserve, wao wakitaka kurudisha uchumi wa marekani nyuma wanazi-print karatasi nyingi tu, na kuzizungusha na matokeo yake economic depression zinatokea, bila hivyo mzunguko wake ungekuwa mdogo, sisi tuna madini lakini sheria zetu za mikataba zinaturudisha nyuma, na sio kwamba hawataki kuzibadilisha lakini kuna conditionalities za world bank na IMF ambazo tukijaribu kuzibadilisha tutaumia sana

[5:27:02 PM] Emmanuel Joatham Kamala: yaani tumeshatawaliwa kwenye mifumo yetu ya kiuchumi kutoka na hizo conditionalities, ni mfumo mmoja unaitwa SAP
[5:27:16 PM] Emmanuel Joatham Kamala: structrual adjustment program

[5:27:34 PM] Emmanuel Joatham Kamala: ambapo tokea kwenye miaka ya 80 ndio tuliingia kwenye huo mkataba ili kuokoa uchumi wa Tz

[5:27:41 PM] Emmanuel Joatham Kamala: ambao ulikuwa unayumba

[5:28:04 PM] Emmanuel Joatham Kamala: Nyerere alishindwa kukubaliana na huo mfumo na alikuwa hana mbinu za kuipinga ikabidi aachie nchi

No comments: