Monday, October 3, 2011

miaka 50 ya uhuru, eti uhuru ni kitu gani?

eti tunasheherekea uhuru wa tanganyika miaka hamsini, hivi uhuru ni kitu gani? eti wewe uko huru? nikiwa kijana wa miaka 30 najiuliza uhuru ni kitu gani hiki kisheherekewacho! CCM inadai ilileta uhuru, eti wewe ambaye hujui ukoloni wa live unaweza kuelewa uhuru ni kitu gani? lakini je uko huru kiasi cha kusheherekea?

hivi kuna taifa africa lililoleta uhuru au ulifika t wakati wa kuwekewa wakoloni weusi wa kututawala? hiv katika jamii iliyojaa kudanganyana, rushwa na kadhalika, waweza sema ina uhuru? eti kuna cha kusherehekea kwenye uhuru?

taifa letu lina kila ugumu, huduma za afya za hovyo, hamna elimu, chakula shida, miundombinu noma, tuko huru?

wakoloni mamboleo wanachukua rasilmali zetu watavyo, tunaingia mikataba ya hovyo eti tuko huru, kuna uhuru hapa?

eti wewe uko huru ndugu? viongozi wanatibiwa nje ya nchi, wanasomesha vijana wao nje, hawakose fedha za kununulia vitu vya anasa kama vile fenicha, maghari, majumba nk, ni kweli wako huru lakini je wewe uko huru?

badala ya kusheherekea uhuru, na sasa tuupiganie uhuru wa kweli. tutafute uhuru wa kwetu, huu tulionao umepitwa na wakati

1 comment:

Munale said...

Uhuru wa kisiasa haujaweza kuzisaidia nchi nyingi za Afrika,tumewafukuza wakoloni tukabaki na mafisadi nadhani sasa ni wakati muafaka wa kupigania uhuru ili tutoke kwenye ukoloni wa mafisadi!