Tuesday, November 1, 2011

imepita mitano ya kuwa kijiweni!!wanakijiwe, ukweli ni kwamba kijiwe hiki kinazidi kula umri. sasa kimefikia miaka tano bora kabisa. kimefunga vidole vitano vya kwanza, swali lililokuwepo mwana jana ni itakuwaje huko mbeleni?? kumbe bado kipo, kinasavaivu freshi tu

kuna mabadiriko mengi kwenye blogu, baadhi zimefungwa na nyingi ziko dormant, mpya zinafunguliwa nk, lakini bwana hii inaendelea fresh tu

sifa na heshima ya kuwepo na kufunga mitano ya kwaza ipo kwako usomaye hapa maana bila watu kama wewe kuwepo, hamna cha miaka mitano wala aandikiwaye haya amini usiamini ndugu

ni mwaka watano wa kuwa na kijiwe hiki. kijiwe oyeeeeee

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kumbe kijiwe hiki ni kikongwe..HONGERA SANA na kidumu milele.

chib said...

Duh, mimi nilifikiri miezi mitano kumbe....
Kila la heri na uendelee na kazi hii ya kuelimisha watu, ili wafikiri na kujadili.

maisha ni mikikimikiki said...

Tano miaka,kijiwe kinang,ara
Kaskazi nako kusi,pongezi pokea
Makini zako fikra,wako wadau wausifu
Tano hii miaka,hongera zetu pokea.

maisha ni mikikimikiki said...

"MAKINI ZAKO FIKRA,WAKO WADAU WAKUSIFU".