Friday, November 25, 2011

KAMA WAHAYA WASINGEBUNI MPANGO WA KULA SENENE, BASI MWAKA HUU NJAA INGETISHIA UHAI


Ndio senene ni kumbe mdogo wa jamii ya panzi. Inasemekana senene hutoka ziwani ambako hulipuka kama kumbi kumbi lakini wataalamu wanasema wakati wa kutoka huwa ni wengi mithili ya mlipuko wa volcano

Wahaya / wenyeji wa mkoa kagera wanakula senene, wanapenda kula senene na senene imekuwa sehemu ya utamaduni wa wahaya. Kwa uchumba, senene ndio pete ya uchumba kwani binti hupeleka senene kwa mume mtarajiwa na mume hupokea, hula na kutoa zawadi ya kanga au kitenge. Wahaya sasa wameambukiza jamii nyingi za kitanzania kula senene. Binafsi sipendelei kula senene kutokana na imani yangu/msimamo wangu wa u- vegetarianism.

Basi mwaka huu senene niwengi na wakutisha kwakweli. Hapo zamani, senene weliweza kutua kwenye mti wa mwembe na kudondosha matawi yake kwa ule wingi na uzito. Senene walitafutwa kienyeji kwa kufukuzwa, kuviziwa na hata kupekua pekua majani porini

Siku hizi maendeleo ya sayansi na teknolojia, hayakuacha senene nyuma. Kuna taa maalumu za umeme zinazovuta senene. Watu hukusanya magunia na magunia kwa muda mfupi. Senene mbichi hupaswa kuuzwa haraka kuisha kwani huharibika wasipotunzwa vizuri.

Vyandaru(hata vile vyenye dawa) sio kinga ya mbu wa malaria tena bali ni dhana muhimu sana ya kukamatia senene. Senene wakitua wengi ni kama nzige. Wanaweza kula mazao na kuyamaliza shambani. Lakini kwa tekknolojia ya kisasa ya kuwavuta kwa mwanga wa taa za umeme, kuwafukuza kwa udi na uvumba, senene hawaonekani kuwa hatari hata kidogo bali ni neema.

Watu wengi mtaani wanamshukuru Yule aitwae Mungu kwa wingi wa senene. Laiti wangelijua kuwa bila kuwatafuna, senene hugeuka kuwa balaa kwao

Watu sasa wanafanya biashara ya senene. Inalipa. Wamenunua magari, wamejenga majumba na kupata mitaji hata kupate wenza wazuri kutokana na senene. Biashara ya senene inazidi kukua hapa nchini na huko Uganda. Biashara hii imetapakaa miji yote mikubwa ya Tanzania bara.

Umuhimu wa teknolojia ni kwamba hata kama senene wana msimu mmoja tu, lakini hupatikana sokoni mwaka mzima. Hapo zamani tulihifadhi senene kwa kuwafunga kwenye kamba / majani ya migomba na kuwaweka juu ya jiko eneo la moshi ili panya na sisimizi wasiingie.

Heri yao walaosenene maana wamewapata, na ole wangu nisiyependa kula senene maana nashuhudia watu wakifurahia chakula/kitoweo au kiburudisho hicho.


6 comments:

tanzaniakwetu said...

Mmh, Kweli huu ni ubunifu ni wa kimataifa, na huu ndiyo unatakiwa kwa kila jamii, kuweza kufanya jambo fulani jipya na kuleta maendeleo kwani mpaka watu kuweza kupata mitaji na kujiendeleza kupitia mradi wa senene ni ajira tosha kabisa.
Tuendelee kuwa wabunifu jamani!

Anonymous said...

wewe na uvejiterian wako unakosa uhondo ingawa hukosi uhondo huo kwa msimamo wako lakini na mimea bado nayo unainyanyasa maana nayo inauhai,wakola muno omubihandiko byawe inkeisheze abaNshamba

Anonymous said...

unanitoa mate kamala kutokula senene una mashariti fulani nini?maana wao ni wadudu sio nyama

Anonymous said...

anamashariti ya mizimu ya kihindi inaitwa bhaggathi

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio, ni wadudu, sitaki. wewe mzimu wa kihindi sio Bhaggathi, labda santmat

Yasinta Ngonyani said...

Nimekula vyakula vingi ila senene kwa kweli sijawahi kuwala itabidi niwatafute