Wednesday, November 23, 2011

Dini zetu, Mungu na kile tukiabuducho

Kuna wanaodai juu ya tofauti kati ya dini na Mungu, Mungu na vitabu vyake na tofauti kati ya vitabu vya dini(vitakatifu?) na dini yenyewe

Katika ukristo, watu wameamua kutumia biblia na kumuabudu Mungu wa kwenye biblia. Mungu huyu ni baba na sifa zake zinaendana kwa kiasi kikubwa na baba zetu wa duniani. Anachikia haraka, anaadhibu, anapiga viboko, anaharibu vibaya, hasira yake ni kali, lakini pia anaupendo.

Mabaya mengi yatokeayo kwa mtizamo wa Mungu wa biblia, ni adhabu, ni onyo na fundisho. Katika ibada, huwa tunaambiwa zaidi juu ya shetani na ghadhabu ya Mungu na kwamba siku za Mwisho kuna adhabu kali itokanayo na hukumu y a Mungu na kuchomwa moto na kuteketea

Mungu wa kiisalamu, haitwi Mungu bali Allah. Huyu ni Mungu, hana jinsia kwa hiyo sio baba (kama wa Bibla) wala mama kama yule wa dini za Asia na nyinginezo. Lakini anamasharti makali pia

Kuna Mungu wa dini za Asia, baadhi ya dini hizi umrejea Mungu kama mama. Mungu huyu anamaelekezo mengi ya kimama, yaani yenye upendo, kulea, kurekebisha, kuvumilia nk kwa ujumla kama vile mama amleavyo mtoto au ampendavyo mtoto. Masharti ya Mungu huyu yana nafuu.

Lakini sasa kuna changamoto juu ya Mungu aliyeandikwa vitabuni na kile tukiabuducho. Watu wameachana na Mungu aliyeandikwa vitabuni na kuanza kuabudu vitu vinginevyo. Kuna wanaoabudu Sanamu za Mungu asiye na sura, wengine huabudi mitume wake kama vile yesu kristo.

Kwa wakristo wengi wanachukua muda mwingi kumsifia Yesu aliyekataa sifa yoyote akiwa duniani. Tafsri ya maneno ya misahafu zimeshindikana kwa akili ya binadamu na hiyvo waumini kuaminishwa kichangamoto zaidi ya uhalisia. Na waumini wengi wamekaa kimya kusubili kutafsiriwa.

Dini nyingi zimegeuka kuwa asasi za kijamii kuliko kuwa pahala pa kukuzia watu kiroho kutokana na ukweli kwamba zinaongozwa na wasomi wa kidunia ambao pia hawajakua kiroho na hivyo kujikuta wakiwa mhanga wa wale wayahubiriayo wengine

‘ego’ nayo imeteka dini, kila dini ni superior mbele ya nyingine, kila dhehebu pia ni superior, hata ndani ya dhebu kuna ubaguzi wa waliozaliwa mara ya pili na ambao bado, charismatic na wasio charismatic nk nk nah ii ni kwa kila dini.

Mahubiri ya siku hizi yamekaa kisiasa na kijasiriamali zaidi. Mafanikio ya nyumba za ibada na viongozi wake hayamo tena kwenye kukuza waumini kiroho bali makusanyo ya fedha. Ni kweli kuna tofauti juu ya Mungu na kile tukiabuducho siku hizi

3 comments:

Anonymous said...

Na hapo ndipo penye hekima mkuu,...kila dini inajikweza juu ya nyingine,..na hasa hizi mbilikama si tatu zenye asili ya Abrahamfe

chib said...

Dini = Biashara

Anonymous said...

hapo umesema nimekuelewa hizi dini ni michosho tu bora dini yangu ya matambiko ambayo haimlazimishi mtu kutoa kwa lazima ni hiyari yako,hivyo haya madini ni michosho tu,bora WAMARA,KASHASILA,BWOGI,NYABINGI,MUGASHA,IRUNGU,NYANJOBE,MUHAYA,OMUKEILE NAWENGINENAWENGINE