Wednesday, November 30, 2011

nyerere na kura za kichaka

jamani nyerere ni mwema na ni mtakatifu. lakini je uliwahi kujiuliza ni kwanini alipenda kugombea na kichaka na sio binadamu mwenzie?? yaani ilikuwepo sura ya nyerere na kichaka kwenye karatasi zakura?

ni kwamba watu wa kushindana naye waliisha au aliamua tu kutumia kichaka kama waoga wa kushindwa? je sio udiktata mtu kugombea na kichaka??

je watanzania wa enzi hizo si walizarauriwa sana kuletewa mtu na kichaka wachague?/ na walijitokeza kupiga kura, sio ujinga huu kweli mtu mwenye akili timamu kugombea na likichaka?

unadhani hii ilikuwa ndio demokrasia? huwa sielewi kitu hiki na umahiri wa nyerere hapa kama sio udikteta hivi kichaka kinaweza kulalamika kuibiwa? kwanini kupiga kura si ameishashinda? sio danganyatoto na kupoteza muda na fedha kwa kuwachonganisha mtu na kichaka je kuna utakatifu katika hili?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mmmhhhh! sina la kusema!

Anonymous said...

kujilinganisha na kichaka nikwamba alikuwa hafai akilizake za kichakachaka na ndio maana nchi ilimshinda,yeye na kichaka sijuikama uliwahi kusikia habari ya chifu mmoja wa kiyanja alikuwa anaitwa Kahigi alikuwa anakwenda na mbwa wake anakaa kwenye daraja moja linaitwa kyabakoba halafu watu wakijakuvuka anasema mpaka olyamye embwa yange{umsalimu mbwa} wangu ndipo utavuka daraja,jamaa mmoja akamwambia iwapo salamu zako za heshima ninazo kuamkia wewe nimwamkie na wewe ni mbwa kwa ujuha wake akacheka kumbe ......

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony! nimeipenda hiyo