Thursday, December 15, 2011

Na ndo maana nikaacha kusheherekea Christmass kwani kila siku ni sikukuu tu

Ni kweli nimezaliwa katika familia ya kikristo iliyonifanya kuwa mmoja wa wanaosheherekea siku kuu iamanikayo kuwa ni ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kiongozi mkuu wa ukristo na labda chimbuko halisi la ukristo duniani na hivyo kujikuta nikiwa mmoja wa wapendao sana kusheherekea siku kuu ya Noel, Christmas au X-Mass kwa kikwetu tuliita Nwelyi badala ya noel

Katika kukua kwangu nilipenda sana na kutamani siku hii inafika. Lakini kila ilipofika na kupita, sikukuimbilia tu luisubilia Nwelyi Nyingine kwa hamu, bali nilichukua muda na kipindi kirefu kutafakari si kuu hiyo. Kwa kweli nilibakia na maswali bila majibu juu ya siku kuu hii, kama vile; mbona hamna tofauti na siku nyingine? Mbona ni yakawaida tu? Mbona hamana jipya? Mboona ni wakati wa viumbe wengine kuteswa na kuuwa ili wawe kitoweo waliwe na binadamu wakati wote wameumbwa na Muumbaji mmoja? Mh

Nikaja kugundua ya kuwa kumbe Nwelyi ni siku kama siku nyingine tu na kumbe siku zote zinalingana na kila siku ni kubwa au ni siku kuu tu kama siku nyingine kwani siku uliyokwisha iona na uliyonayo ndiyo kuu kuliko ijayo na ile iliyopita. Kumbe Nwelyi ni siku ya kuomboleza wale wanyama wafao ili binadamu afurahia na kkumtukuza Mungu wake.

Kumbe hata maandiko ya biblia ambayo wakristo wengi hadai kuyafuata, hamnaga habari za kusheherekea siku kuu ya kuzaliwa kwa Yesu bali angalau imetajwa ile ya kufa (fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu). Kumbe hata siku aliyozaliwa yesu ina utata kuliko uhalisia kama kweli ni 25 dec nk nk

Ndo maana basi niaachana na biashara ya kusheherekea siku kuu kwani nasheherekea kila siku kwa kuwa kila siku ni kubwa tu hamna inayozidi nyingine ukuu na labda zile ziitwazo sikukuu ni wakati mwafaka wa kuomboleza vifo vya wanyama kwa ajili ya sherehe ya binadamu

2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

"Ndo maana basi niaachana na [BIASHARA] ya kusheherekea siku kuu..."

Na kweli ni biashara tu, naye Yesu au Mungu ni kisingizio kama binadamu anavyofanyaga si kuwachinja wanyama tu lakini hata binadamu wenzake anatoa roho kwa maelfu kwa kudai eti vita nayo ni ya Mungu au ni tukufu, Jihad!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

si ndo apo