Friday, January 13, 2012

kusaidiana maishani

watu hupenda kuwasaidia wale tu wanaojuana nao. lakini binadamu twapaswa kusaidiana. kuna wanaojibagua na kuamini kuwa wako salama wao peke yao na kujiaminisha kuwa hawahitaji msaada wa wengine. lakini kuna wanaosaidia kundi fulani tu ambalo wanajua linaweza kuwasaidia pia na hivyo ni kama wanalinda msaada wao kwa kundi hilo

ukipata ajali ukalaliwa na gari lako zuri, au ukuta wanyumba ukikulalia kama sio nyumba kuwaka moto, huwa unaita, Msaadaaa, msaadaa, msaadaa! je unamiwta nani mwenye msaada? si umekamilika? jisaidie mwenyewe! hii inaonyesha kuwa kumbe watu wengine ni muhimu kama sisi au kuzidi sisi ndo maana tunaitaga msaada na sio kujisaidia sisi wenyewe

kinachoshangaza ni pale watu waliowahi kusaidiwa maishani, wanapoona wivu au kuzuia wengine wasisaidiwe! inashangaza kidogo hii japo wao hufurahia kusaidiwa, hawataki wengine wapate furaha hiyo pia!
saidia tu mzee

No comments: