Tuesday, January 17, 2012

mtu aliyekusaidia lakini unalazimika kuwa mbali naye

ndio ni kawaida maishani kwamba watu waliowahi kutusaidia na kufanya historia zetu kuwa zilivyo au nzuri zaidi huwa tunajihisi kutoa fadhila angalau kwa kudumisha urafiki / ukaribu nao kwa njia za kutembeleana, kusamilimiana, kuwasiliana na hata kuheshimiana

lakini hufika hatua watu waliowahi kukusaidia unalazimika hata kuwakwepa hata kutokungea nao. kuna ambao wanataka kila mtu atambue kuwa aliwahi kukusaidia, laikini kuna waliokusaidia ukapiga hatua mbele lakini unaona kama hawataki usonge mbele. hapo maswali huzuka juu ya msaada waliowahipatia wewe, walilazimika? walitafuta jina? au walikwepa aibu ya jamii? mbona wanakuwa hivi?

basi wakatai mwingine wajikuta ulazimika kuwa mbali na hata kuwakwepa kabisa ikibidi

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Kamala kwa mada hii ya kufunza. Hii ni mara nyingi aliyepata husahau mapema kuliko aliyetoa.

SIMON KITURURU said...

Msaada ili baadaye mtu ajigambe sio msaada huo.


NYONGEZA KIBIONGO:
Huwa nawastukia sana tu watoao misaada ambao unahisi wanafanya hivyo kwa kuhisi watatokea kwenye TV!:-(