Monday, January 9, 2012

ndio nimerudi tu

nimetoka shambani baada ya likizo ya wengi kusheherekea sikukuu. mimi nilipata wasaa mwafaka kuhudhuria shamba langu na kuliweka sawa tayari kwa kupanda na kuvuna. nimetumia likizo yangu vyema kushiriki kazi hii. natamani itokee likizo nyingine ya haraka nikapanue shamba. nifurahie kilimo na mavuno yaje kuwa mengi mazuri ya kuvutia

ndio nimerudi kwenye minyororo ya kufungwa na nisichopenda kukifanya kisa chanipatia shilingi mbili tatu ya kuwekeza shambani kwangu. eti unanidai kukupongeza na mwaka mpya? upi? kipya nii kipi? si utazeeka soon huu au? haya Hongera kama wanilazimisha

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

anayelima ni mmoja ila walaji ni wengi..kwa hiyo utakapokaribia muda wa kuvuna nialike. Na halafu karibu sana

Goodman Manyanya Phiri said...

Karibu tena!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mwakola