Friday, January 27, 2012

penye maumivu ni maumivu zaidi ili pasiwe na maumivu

kuna vitu vinavyoweza kushangaza kwamba ili kutibu maumivu ni bora kuongeza maumivu zaidi japo kuwa kuna dhana ya upendo na unyeyekevu kama dawa ya ukali zaidi kama alivyofanya dogo janja nabii Issa.

kwa mfano, Daktari akipilekewa mngonjwa mwenye homa mwili mzimo, humuongezea kwanza sindano ili aumie zaidi na aje kupona! je ile sindano yaponya au yale maumivu ya sinda yaliyomaradufu ya aliyokuwa nayo mgonjwa humfanya mgonjwa kuyasahau aliyonayo na kukumbuka ya sindano tu ili apone??

hata dwa za vidonge za kidhungu kwa mfano; tuliotumiaga kororokwini (chloroquine) enzi zile tunajua uchungu wa hii dawa na muwasho wa kujikuna. hii ulipewa uliponda hospital unaumwa na labda huwezi hata kula, jibu lake unapewa vidonge vichungu, unatapika na nini sijui ili uje kukumbuka utamu wa vyakula unavyozila kwa sababu ya ugonjwa!

ndio maana mwanafunzi huambiwa habari za kushindwa na ubaya wake kuliko uzuri wa kushinda mitihani ili atafute uzuri huo. kubwa zaidi na kwenye nyumba za ibada zenye lengo la kupeleka watendamema mbiguni. katika nyumba hizi vitu vibaya huongelewa zaidi. yaani shetani uongelewa kanisani na kutawala kuliko yesu mwenyewe.

habari za jehanamu hutawala kuliko zile za akhera. hata barabarani habari za ajali hutawala zile za safari yenye usalama. hata kwenye ndoa vitisho kama vile vya kuachana kuliko kuishi pamoja milele. tahadhari zote huongelea mabaya zaidi na makali. yote ni malengo ya kutengeneza/kujenga uzuri zaidi

kwahiyo tusemeje hapa?? madaktari wanapaswa kuwa na roho mbaya ili wagonjwa wapone? ndiyo kwani niliwagopa sana madaktari udogoni hata kama ni wasafi kwa nje. au je wahubiri wanamjua shetani na labda wana ukaribu naye kuliko mungu ili waweze hubiria taifa liokoke? ndio kwani humuongelea shetani zaidi.

binadamu ni vigumu kujifunza na kuacha tabia mbaya bila maumivu na akiweza kukwepa tabia hiyo mbaya ujua kajifunza kutokana na maumivu aliyopate mwenzie au kusoma sehemu. kama hutaki shauri yako. ubaya wa ukimwi ndio hufanya watu kuvaa kondomu na kuukwepa uzinzi, huamini?

maumivu jama

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Maumivu sijui ni vipi nianze...maana kuna maumivu ya aina nyingi sana na yanayoumiza kweli..ngoja ntarudi

SIMON KITURURU said...

DUH!