Friday, February 24, 2012

Katika kuhitaji break ya maisha

Kuna vitu vingine bwana viko kihajabu. Wanyama wote hukimbia au hutembea kwa spid ili kuwahi sehemu, laikini hufikia mahala pa kuhitaji break. Vimetengenezwa vifaa vya kumkimbiza binadamu zaidi kama vile baiskeli, pikipiki na hata gari, lakini hufikia pahala vinawekwa break yaani kuzuizi cha kukimbia wakati kazi yake ni kukimbiza

Twaweza jisifu kuwa break hutumika pale kukimbia kukiishaishiwa maana yaani kusimama au kuacha kukimbia kabisa, lakini sio kila tubanapo break huwa tunataka kusimama. Tunafunga break sehemu harafu tunaongeza mwendo baada ya kuachia break.

Labda na maisha ndivyo yalivyo kwani tunakuwa wazima wa afya then wagonjwa tahaban, tunalala ili tuamke na tunaamka ili tulala. Tupumzika harafu tunafanya kazi ili tuchoke tupumzike tena.

No comments: