Tuesday, February 14, 2012

social issues -- sasa wakatoliki waja na ndoa mseto

kuna masuala ya kijamii, ni magumu kuliko maelezo. ndio kwenye familia ndoa Nk


mmesikia hii ya kupunguza masharti ya dini??

eti kanisa Katoliki (KK) limeruhusu ndoa mseto, yaani ndoa kati ya mkatoliki na muisilamu. zamani ilikuwa zambi hata mkatoliki kuoana na mkristo mwenzie. sasa kimekuja kizazi chetu kisichotanguliza dini kwenye mambo yake hasa ya ndoa jamaa wameona badala ya kupoteza waruhusu jamaa waone

je kweli ndoa kati ya dini tofauti ni dhambi? bila shaka hapana. leo hii kwenda na wakati imeruhusiwa. je waweza kumuacha umpendaye kisa kiongozi wako wa dini hataki? utakuwa chizi fulani au humpendi kweli

wakatoliki sasa mko huru kuoa waislamu, hongera

4 comments:

Anonymous said...

wacha waoane haina tabu ila bado mapadri nao inabidi waoe sio waendelee kuwa wasela{wahuni}

Goodman Manyanya Phiri said...

Dini ni ya kumtumikia binadamu; wala sio binadamu kuitumikia dini. (Hata maana ya Mungu inategemea kuwepo kwa binadamu).


Au niseme: wale wanaotaka kutawala mambo ya ndoa za binadamu kutokana na dini au dhehebu, NI WAGONJWA WA KICHWA TU, wala si wachamungu!

Anonymous said...

sawa goodman umeongea la maana sana

chib said...

Mbona ndoa mseto ipo miaka mingi tu kwa wakatoliki, kilichokuwa kinasisitizwa ni kuwa mwanaume ndio lazima awe mkatoliki ili ndoa ifungwe kwenye kanisa katoliki....we ndio umeisikia siku hizi