Thursday, February 23, 2012

Upendo ni ukweli wa ndani ya moyo. Upendo ni msukumo wa ndani na si nje. Maana ya upendo huanza ndani ya mtu na kila mtu anao uzuri wa ndani uliobeba upendo ; hata kama mtu huyo anafanya mabaya kiasi gani, au hata kama anaonekana mbaya kimatendo – mimi naamini kabisa kuwa kila mmoja wetu anayo mazuri ndani mwake, mazuri yaliyobeba upendo.
Upendo ni hali ya mmoja kujitoa kwa faida ya ampendaye bila kudai fidia au malipo. Kwangu mimi: Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya.Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli.Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.Upendo hauna mwisho.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimeipenda hii kamala tena mno Ahsante kwa hii mada na nitaiomba niiweke jumatano kama marudio. Upendo daima:-)

Anonymous said...

sawa kamala imekomaa hiyo batamwa