Wednesday, March 14, 2012

HIVI NDO VIOJA TUNAVYOPATA KWENYE DALADALA WENZENU TUSIO NA MAGARI!


Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!?
Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado
hajatoa album...
Abiria: "Kuna Kiti au unasema
panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia
ndoo?! "
Abiria: "Embu punguzeni sauti ya
redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu
zinatushinda, tusikilize na zako!?
hebu tupunguzie misheria"
Mmama: "Bwana ondoa gari joto
sana!!"
Konda: "Usituzingue wewe,
shukaupande fridge...."
Konda: "Anti, kuna siti pale
nyuma,ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe,
Kwani za nyuma ziko nje ya
gari?!"
Sister duu: "Konda unanibana
bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa
huzisemi, kama ulitaka kujiachia
ungekodi treni peke ya
Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama
hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa
kiti si ungebeba chako!!?"

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Jamani jamani mpaka hamu ya kusafiri inakwisha labda tuanze kutumia baiskeli...