Tuesday, March 6, 2012

MSONGO, HASIRA

wanasema hasira, mawazo mengi nk vyaweza kuleta au kusababisha msongo mkubwa kwa yule mwenye hasira. hii usababishwa zaidi na kutokupata matokeo halisi ya matarajio. umsikini au kipato kidogo, utegemezi na hata wingi wa vitu vyaeza kusababisha msongo

msongo ni ile hali mbaya ya kuwa na hasira na kutokujua nini cha kufanya wakati huo. ni khali ya kusikia /kuhisi akili imejaa au kichwa kimejaa na hakuna suruhisho au jibu la maswali mtu aliyonayo. yaweza kuwa hata wingi wa mahitaji au zaidi ya hayo na kuona maisha hayana maana tena.

dawa kuu ya msongo yaweza kuwa tahajudi au meditation japo kukaa na wengine, kupiga stori, kusikiliza muziki nk vyaweza kupunguza hali hii kama sio kuiondoa kabisa. ila msongo ni noma. waweza ona mtu anamtwanga paka teke, au anagonga mawe njiana atembeapo, anatoa matusi na kukushambulia bila sababu. hii yote ni uchizi uletwao na msongo. wengine hunywa sumu na kufa kabisa au hujaribu kujiua.

No comments: