Tuesday, March 20, 2012

Mwanzo wa nahusiano ya jinsia tofauti.


Uumbaji umefanyika kwa jinsia mbili tofauti katika viumbe vingi na zaidi wanyama akiwemo binadamu. Mzee Lubaju wa Bukoba aliwahi kuniambia ya kuwa ukiulizwa swali tangu asubuhi umekutana na watu wanganpi, jibu ni fupi, wawili yaani mwanamke na mwana mume.

Tunazaliwa tukiwa watoto wadogo. Tunakua tukiwa tumejifungamanisha sana na wazazi wetu, baadae ndugu zetu. Taratibu, huja wakati wa kutafuta mahusiano na watu wengine wasio kuwa sehemu ya familia zetu na hata ukoo wetu. Hawa ni marafiki wa jinsia tofauti, maraiki wa kike/kiume ambao baadae huzaa mapenzi baadae uchumba hadi ndoa

Japokuwa safari ya kuanzia kwenye urafiki mpaka kwenye ndoa ni ndefu yenye milima na mabonde, lakini hayo ndiyo maisha yenyewe na mfumo ulioumbwa kuwa hivyo. Kijana wa kiume alikuwa akiwapenda ndugu zake wa kike akiwemo mama, taratibu huanza kumtafuta rafiki wa kike, vivyo hivyo kwa kijana wa kike.

Mwanzo wa mahusiano huwa na changamoto nyingi. Wengi hujihisi wamefika, hujiona kama vile wamepata mwenza wa thamani sana japo kuwa tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wapenzi wa kwanza mara nyingi huwa hawafiki kwenye ndoa. Katika kipindi hiki hisia huwa kali sana kati ya wapendanao hawa.

Wengi huanza mahusiano mapema sana, jambo linaloleteleza matatizo huko mbeleni kutokana na ukosefu wa mafundisho mazuri ya suala hili. Katika mahusiano haya ya mwanzo mara nyingi huwa hayaoni milima wala mabonde katika safari yao bali huona mteremko zaidi, hii husababisha ukosefu wa mafundisho juu ya kukabiliana na mabonde hayo kwani elimu ya mahusiano katika kipindi hiki huwekwa pembeni kabisa

Uhitaji wa mahusiano unaonekana kuwa wa kiasili zaidi kuliko kuigwa. Itaendelea……..

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Darasa hili ni tamu sana ..nasub iri muendelezo...

Anonymous said...

sawa kabisa kamala kuna mzee mmoja wa kichaga sikumoja alisimama pale mvinjeni akasema tangu nimesimama hapa nimeona watu wawilitu.... watu wakamshangaaa!!!! akasema anapita mwanamke na mwanamme tu...wacha awavunje mbavu watu ila alikuwa mchekeshaji sana.