Friday, March 2, 2012

NGUVU TUNAZOTOA ZINATURUDIA

jamani sisi kama binadamu ni nguvu na nisehemu ya nguvu kuu yani Mungu. wanasayansi hudai ya kuwa nguvu haiwezi kupindishwa wala kuharibiwa. basi katika maneno, mawazo na matendo tunatoa nguvu ambayo baadae huturudia.

tunakuwa wanafiki na kuwadhuru wengine, lakini baada ya muda itakuwa aibu kwetu na ni katika maisha haya kabla ya kuuaacha mwili nguvu hii itaturudia tu na hurudi ikiwa kubwa zaidi imejizidisha mara na mara.

kauli zetu nimejaa laana, wivu, masengenyo na roho mbaya tukidhani tunafanya vyema, itachukua muda lakini zitatutrudia, kama ni za kuumiza, tutaumia wengine.

tujitahidi kutoa nguvu nzuri kwe wengine. tusilaami, kukashfu, kutukana na hata kusingizia. tupende, tusaidie, tuchukulie na tusamehe. kwani tuwatendeayo wengine, tutatendewa na sisi kwa njia moja au nyingine tena kubwa zaidi ya tuliyoitoa/tuliyoizalisha.

nashangaa kwanini somo hili halieleweki kwa wengi wetu