Friday, March 9, 2012

Ushauri kwa mdada mwenye umri wa kolewa lakini bado kumpata mwenza

Ndo hivyo muhimu ni kuwa na imani katika kile ukiaminicho. Ni kuongeza muda wa kusali na kuomba ili kumtegemeza Mungu zaidi kuliko ku-develop depression isiyokuwa ya msingi. Lakini pia usije jikuta unaingia kwenye ndoa na uhusiano na mtu usiyempenda eti labda kwa kuwa tu unatamani na unahitaji kuolewa. Hii itakuwa hatari na lengo lako la kuingia kwenye ndoa litakuwa hatari na kuleteleza maisha magumu maana hautakuwa umeingia kwenye ndoa kwa mapenzi/mpango wa Mungu balli kwa matazamio yako

Ni lazima sote tuingie kwenye ndoa? Wakati mwingine ni swali gumu la kujiuliza. Lipi bora kati ya kuingia kwenye ndoa ngumu na kuishi maisha ya lawama na vurugu zaidi au kuishi peke yako ukapeleka maisha yako vile wewe unataka kwa amani na utulivu?. Pamoja na maswali hay a najua kuna changamoto kubwa sana ya mtu kuishi peke yako na haswa kwenye single parenting. Hii huleta matatizo ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto walelewao hivyo.

Kwakweli kuwa kwenye mahusiano na kwenye ndoa ni jambo jema na zuri endapo utapata Mr Right. Kwakweli maisha ya ndoa yanapendeza. Ni mazuri, ni kushirikiana na kushirikishana ambapo ndio ubinadamu wenyewe

Unachohitaji ni kumomba Mungu kwa njia zako na kwa imani yako., ongeza muda wa kuomba ili kujikabidhi mikononi mwa Mungu ili mpango wake kwako ukamilike ili upate mwenza ambaye ni mpango wake kwako.

Usiwe very anxious sana kumuona huyo utakayeoana naye haraka, balli mwachie Mungu akuonyeshe na kukuletea mwenyewe kwa njia zake ajuavyo na atakavyo. Muhimu ni kupata muda wa kukaribisha uwepo wa Mungu kupitia maombi, kusoma maneno ya Mungu/yenye Busara na tafakuri ya kina (meditation). Then utajua tu na utakuwa tayari kupokea hari yoyote ile kama ni kupata mwenza wa kuishi naye au kupata tu mzazi mwenza yaani mtu wa kuzaa naye tu

Kamwe usipoteza muda kwa kuruhusu mawazo hasi ya kukuletea msongo (stress) na depression. Kila ujisikiapo kuwa na mawazo hasi juu ya maisha yako, then mkaribishe Mungu kupitia maombi, tafakuri na kusoma maneno yenye busara / matakatifu. Ni vyema kutokusubiria hari hizi zikutawale na badala yake kuishi kwenye uwepo wa Mungu iwe tabia yako ya kila siku.

Jikubali. Ishi utakavyo na kubaliana na hali yoyote ile. Usijilinganishe sana na wenzako kwamba Fulani kanizidi kwa kuwa kaolewa au ana watoto kadhaa. Jipokee ulivyo na kubaliana na hari ilivyo na endelea na maisha yako ya amani.

Love and peace

Kamala Lutatinisibwa

5 comments:

Simon Kitururu said...

Tatizo la kuomba MUNGU - hata vitani majeshi yote huomba MUNGU kwahiyo labda MUNGU akiombwa majibu yake MBABE hushinda.
Ushauri wangu kwa usieolewa kuwa NGANGARi kivyako kama BINADAMU!
Maana mambo mengine kama KUOA na KUOLEWA kibinadamu ni vitu vilivyo tungwa tu na BINADAMU .

Adamu na HAWA tunda tu walistukia wenyewe. Na baada ya kufukuzwa kwenye kigadeni hakukuwa na SHEKHE wala PADRE wa kuvalisha nanihii kidoleni. Samahani nawaza tu kwa sauti na RUKSA kutosikiliza!Na nimeacha!

Anonymous said...

safi saimon kitururu nikiona watu wanahaingaika sijui hujafunga ndoa ya kanisani au msikitini hayo hayakuwepo wewe pata bwana au binti chukua kula vyako au kula kitu roho inapenda

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kwa kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo unavyozidi kukomaa zaidi katika uwanja wako. Hili ni jambo jema!

Ushauri mzuri. Mimi nilipompata wa kwangu aliniambia kuwa alikuwa hahitaji harusi wala nini. Ruhusa na mibaraka ya wazazi wake na ndugu zake tu ilikuwa yatosha. Nilijiona kuwa nina bahati ya mtende kwani niliweza kukwepa migharama ya maharusi haya yanayofungwa...

Anonymous said...

meressmie kila siku namwomba Mungu nami anisikie kilio changu cos nina miaka 30 hata boyfrend wa maana sina. ehee Mungu nisikie

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

take it easy, ushauri ndo kama ujumbe mwenyewe na tuwasiliane labda