Friday, April 20, 2012

MANJONJO YA WAHAYA

Baada ya kumaliza degree yake ya sheria mlimani Bwana Rwegoshora
aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya
kuhudumia clients(wateja) .
... Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana
mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake.Hapo ndipo alipoanza
kunyanyua mkono wa simu ya TTCL,wakati anajizungusha kwenye viti virefu.

Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha
wakati anaongea na simu,alisikika akiongea ''No.no
Absolutely no, You tell those clowns in New York that I won't settle
this case for less than one million. (pause)

Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next
week, I'll be handling the primary argument and the other members of my
team will provide support. Okay. Pliz dont forget to tell the State
Prosecutor that I'll meet with him next week to discuss the details."
Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga
kwamuda zaidi dakika 5.

Baada ya kumaliza kuongea na simu,bwana Rwegoshora alielekea kwa
huyu jamaa.
''Samahani sana, kwa kukupotezea muda wako, unajua tena kazi
zetu hizi unaumiza kichwa sana,kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani
niko busy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe. enh by the way,
what can i do for you?Jamaa alijibu.
'' Mimi ni mfanyakazi wa TTCL,nimekuja kuunganisha line yako ya
simu kwani haipo hewani''

3 comments:

emu-three said...

Hahaha jamani uwongo mbaya sana...kwanini tusiwe wakweli...mmmh, naona hata wazo langu la leo nimekita huko huko

Mija Shija Sayi said...

Hahahahaaaa.. hii ya leo kali sana, hata sijui aliyeyusha vipi situation baada ya hapo...duh!

Yasinta Ngonyani said...

kaaaazi kwelikweli !!!