Tuesday, April 3, 2012

Mwanzo wa mahusiano…

Makuzi yanaendelea, kijana wa kiume aliyempenda sana mama yake na pia dada zake, anaanza sasa kutafuta upendo mwingine. Hata binti aliykuwa karibu sana na babayake, naye anaanza kutafuta upendo mwingine. Ni upendo wenye kuhusisha hisia na ashiki. Vijana wa kiume pamoja na kubadilika maumbile, huanza kuunguruma, utanashati huzuka, huvaa vizuri na kujiangalia mara mbili mbili kabla ya kutoka nyumbani. Wengine hutembea kwa kudunda/kuringa na kuwahiga wazazi wao wa kiume

Mabinti nao huanza kuwa warembo, kuhisi aibu na wenye kujiriemba. Wanasema penye mizoga ndipo tai watakapoelekea, vijana huanza kusaka jinsia tofauti. Katika hatua hizi za mwanzo, vijana huwa na matumaini makubwa. Huhisi kuwa wao ndio wao na mahusiano yao mapya yatadumu milele. Hupenda kujionyesha kama vile wao ndio wajuao kupenda kuliko wote dunia hii. Wengi katika nyakati hizo zamwanzo, hupenda kutembea kwa kushikana mikono na hatakupigana mabusu hadharani

Hukimbilia kufanya tendo la ndoa, hata kama katika jamii zetu tendo hili halifundishwi kwa vijana na limekaa kimkwara zaidi jambo ambalo hufanya kuwa siri kubwa na kulifanya bila elimu yoyote na labda laweza kuwa maumivu zaidi. Vijana huanza kuona mengi na kujifunza mambo tofauti hapa
Huja hatua za kutaka kujaribu jaribu, kuchovya na hata kushindania masuala haya. Itaendelea….

1 comment:

emu-three said...

kazi kwelikweli mkuu, ulezi sio mchezo, ukizingatia huu utando wa wazi