Friday, May 18, 2012

english ni noma wakati mwingine

Mshikaji mmoja alikuwa na dingi yake, akamwona demu wake anakuja, bahati mbaya dingi alikua mkali sana, ili kuua soo, mazungumzo yao yalikuwa kama hivi:

MSHIKAJI: Umekuja kuchukua kile kitabu cha, speak English, my father doesn't know?

DEMU: Yeah! Na kile cha where should I wait 4 u?

MSHIKAJI: Dah! Hicho hakipo, labda kile cha wait 4 me under the coconut tree

DEMU: Sawa, ila usisahau na kile cha I am giving u 10 minutes

MSHIKAJI: Yeah, nita...ta...kupa na kile cha I won't let u down

DINGI: Mbona vingi sana, atavisoma kweli?

MSHIKAJI: Aahh! Huyu anasoma sana vitabu na ndio anatuongoza darasani.

DINGI: Mpe basi na kile cha I am not that much stupid na kile cha I have understood everything u spoke

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ujanja huo ama kweli watu wajanja...najiuliza hivi kweli baba alielewa hapo?

batamwa said...

dada,Yasinta baba ameelewa si unaona setensi hiyo ya mwisho.....alivyomjibu

batamwa said...

samahani dada Yasinta kumbe huu uwanja sio wanyumbani kwako nimedandia tereni kwa mbele