Tuesday, May 8, 2012

Munga Tehenan, ni mwaka mwingine wa kifo chake

ni kweli, huyu bwana alikuwa wa aiana yake, mwaka 2007 alibadilisha maisha yangu kabisa na kunifanya nijitambue. namshukuru huyu bwana na kufurahia maisha kutokana na mafundisho yake. nashindwa kumlilia kutokana kifo chake kwani aliniaga kuwa ataondoka (kufa?) na kuniambia kuwa nisilie kwani kuondoka kwake ni furaha na sio mateso. alikomesha hisia za kulia na badala yake kufikiri

Munga Tehenan, sitomsahau milele huyu bwana. ni kweli jumamosi iliyopita, imetimia miaka 4 tangu huyu jamaa aondoke mwilini. alituaga tusimuelewe tulikuja kuelewa baada ya kuondoka kwake. hata hivyo, namshukuru japo hapendi shukuruni hizi kwa kunibadilisha kwani aliamini ni wajibu wake nakuwa nilijibadili mwenyewe na sio yeye. roho hii ya unyenyekevu, sitoisahau milele.

nitayaishi yoote aliyonifundisha na kuwagawia wengine

No comments: