Monday, May 14, 2012

niliwahi kutoa maoni haya juu ya uafrika

tunapojadili masuala kama haya inabidi tuwe makini sana badala ya kujilaumu na kujiona wajinga, tuangalie uhalisia wa mambo. mimi sio msomi kama nyie na sijaenda ulaya japo sipatamani sana lakini tusiungane na wazungu kujionyesha kwamba hatuwezi lolote. kuna sehemu nimesoma kwamba chuo kikuu cha kwnza kilikuwa misri na mpaka sasa kuna vitu vya ajabu kwenye library za nchini mali. kijijini kwentu yamegundulika maandiko ya zaidi ya miaka 2000 kwenye miamba. inabidi mjue jinsi wakoloni walivyokata mikono na kuwauwa wanasayansi wetu aka wachonga vyuma.

kule kwetu BKB kuna nguo za mabaka ya miti, viatu vya miti na migomba na kuna nyumba nzuri za asili. vibuyu vizuri vya kunyweo pombe maji nk na kuna nyumba zilizojengwa kwa nyansi, udongo, miti nk.

pia tuna mitumbwi ya miti, pombe ya ndizi (lubisi) nk.

haya na mengine mengi hatukufundishwa na mzungu yeyote. hata hivyo mkumbuke kwamba tuliishi tangu dunia kuumbwa bila mzungu kuja africa wala nini na maisha yalikuwa mazuri na tulikula vyakula vya asili na kutumia madawa ya asili bila kuwa na side-effects. hata vifaa vyetu havikuwa na side effects na hatakuleta matatizo kama global warming.

mpaka sasa sisi bado tunaamini katika utu, umoja, undugu nk. ninyi milosoma na kwenda nje inabidi mjue kabisa kwamba mliyoyasoma na mnayoendelea kuyasoma ni mawazo, mitizamo nk vya wazungu ambao wanawajengea picha ya kujidharau ili muwatumikia bila swali!!

kaeni ulaya na US sisi tunaishi pia. kama waafrica hatutamani sana mali kwani tunajua mali zinaachwa lakini "utu" tunaondoka nao. tofauti yako wewe msomi na mzee wa Bugandika au bugabo ni kwamba wewe unaishi maisha ya wasiwasi na hofu wakati yule wa kijijini katulia na ana amani ya kutosha!

hata imani zetu ni nzuri ukilinganisha na za wazungu. soma makala ya padri kalugendo juu ya wamisionari wa ulaya na mungu wa watu weusi.

kauli zenu za kisomi kama hizi, zaweza kunifukuza mahali hapa kwenye blogu hii kama mtaendelea kuangalia uafrika wetu kwa mkabala wa kizungu tu kwamba nyie mnajua upande mmoja tu.

OKOKENI MUNGU WA WAISRAEL ANAKARIBIA KURUDI WAKATI WA WAAFRIKA YUPO NA HAKUWAHI KUONDOKA! ANATUPENDA!

3 comments:

emu-three said...

OKOKENI MUNGU WA WAISRAEL ANAKARIBIA KURUDI WAKATI WA WAAFRIKA YUPO NA HAKUWAHI KUONDOKA! ANATUPENDA!
Hii kali, najiuliza hilo neno `mungu wa WAISRAEL'...!!!

Anonymous said...

kamala asante hapo ndipo ninapokupendea kusema the real thing,kweli hawawanaoishi ulaya ni hofu tuputu.

batamwa said...

halafu mungu niwa waisraeli ni mungu wa yakobo na ibrahim je sio mungu wa kamala na btamwa? ukisema hivyo eti huyo ni shetani sio mungu sijui kwanini?