Wednesday, May 16, 2012

tucheke kanisani

kuna mchungaji mmoja katika mahubiri yake huwa anachangamsha sana waumini wake,kwa mfano utakuta katikati ya mahubiri utasikia "..Muambie jirani yako..Yesu anakupenda!" basi kwa furaha na mbwembwe kila mtu atamuambia
  jirani yake,kisha mchungaji anasema "pokea upendo wa bwanaa!"..Sasa siku hiyo mchungaji alikuwa anahubiri kuhusu wanawake wasiopata watoto,sasa katikati ya mahubiri akasema "...Muambie jirani yako,mwaka huu utapata
  mimba!" bila kujali watu wamekaa na nani jirani wengi walikaa kimya kwani unakuta wengine walikuwa wamepakana wanaume tupu.Mara ikasikika tu mtu kapigwa kofi huko nyuma halafu mtoto akaanza kulia ile kunageuka wanakutana> na baba akimwambia mwanae wa kiume "..
Ukome!".Watu wote kanisani mbavu ziligongana kwa kicheko.

2 comments:

emu-three said...

Nimecheka kweli, nawashukuru hawa wahubiri maana siku hizi kila kona wapo, wanawapasha watu `live'...

Anonymous said...

huo ndio utapeli wa sasahivi na usaniii na watu wanafurahia