Saturday, June 9, 2012

JERRY MURO ATANGAZA KITUO CHA TV ATAKACHOANZA KUFANYA NACHO KAZI.

Jerry Muro Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa muda TBC alikokua akifanya kazi.
Jerry amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.
Kuhusu kuendelea kutoa habari zake za kufichua maovu, Jerry amesema “ni kazi ambayo iko kwenye damu yangu unajua watu wanaweka matuta barabarani lengo ni kufika mbali japo utafika sehemu utapunguza spidi unaruka tuta unakwenda, sasa hivi tutaifanya kwa ubora zaidi lakini pia sio siku zote tu tuchunguze chunguze kuna saa nyingine inabidi utoe breki alafu uangalie”
Kwenye sentensi nyingine Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.
“Sio kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri zitajitokeza basi zitapewa nafasi”Jerry Muro

No comments: