Friday, July 6, 2012

KWELI; Kweli ni nini?Ingawa kuna majibu mengi ya swali hili lakini nina hakika kwamba sisi- watu tuko hapa katika dunia ili tuweze kujifunza, kuchunguza na kufanya kazi ndani ya mzingo wa Kweli.
U-asi katika ulimwengu upo kutokana na ukosefu wa ufahamu wa Kweli,

Kweli ni mahusiano ya kiuwiano kati ya Muumba na asili na pia mahusiano ya kiuwiano ndani ya asili yenyewe. Asili huwakilishwa na falme nne; falme ya Madini, falme ya Mimea, falme ya Wanyama na falme ya Binadamu

Kweli haibadiriki, kweli haipishani, kweli haina mbadala, kweli imezingwa ndani ya na ni kiini cha asili.
Madhumuni ya awali ya taasisi zote za kiroho / kidini ulikuwa kuongoza mtu kwenye ufaham wa Kweli.
Muumba wetu; Mungu hutupa majukumu akiangalia uelewa wetu wa kweli na tendaweza yetu ndani ya hiyo kweli katika kutekeleza majukumu yetu kiulimwengu.

QQ –
Kiasi gani tumefanikiwa kufahamu kweli katika kipindi cha miaka elfu mbili iliyopita na ni kiasi gani zaidi tunahitaji kufanikisha. Je katika ufahamu tumepanda au tumeshuka ngazi?

No comments: