Tuesday, September 25, 2012

mkuu wa din anapodhalilishwa

limwengu majaaa majanga, 
vitimbi vituko chekesho.
kama hapana amaini
ona mwenyewe machoni

kadhaliishwa aliyetutumwa rabuka
binadamu paswaye okoa,
kataa oklewa dharau
weka pesa tokomeza kabisa

shangaa jinsi dhalilishwa,
enye sifa lukuki ahera,
zaidi ya binadamu baki
wezaje dhalilishwa naye?

piga hua balozi wa taifa,
lotengeza filamu dhalimu,
Mungu hesabuje hiyo?
auwaye kwaniaba yake.

Si maulana jalia pumzi?
kwanini siminyie hewa ife?
badalaye tuma wewe silaha,
hua kwaniaba yake?


na Kamala J lutatinisibwa

1 comment:

emu-three said...

Mkuu shati jeupe, katu halipati doa.