Tuesday, October 30, 2012

kwa nini kuhitaji kile badala ya ulichonacho

Mambo mengi tuyafanyayo na au tuyaishiyo sio halisi kiukweli. Maisha yetu ni kama maigizo au labda ndio mfumo wenyewe ulioandaliwa?

Vilitengezwa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kupepeleka watu na vitu haraka kama vile gari, baiskeli na pikipiki, ajabu ni vifaa hivi kuwekewa break ya kuvizuia kwenda haraka. Ndio kazi ya break sio kusimama tu bali kuzuia vifaa vilivyotengenezwa kwenda haraka visiende haraka!
Tujenga nyumba na kweka madirisha ili tuwe kama walionje. Tunakula chakula ili tushibe kumbe hitaji sio kushiba tu. Tunaserikali inayoongozwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa kura nyingi na inasemekana viongozi hawa wanapendwa zaidi, laikini wanalindwa dhidi ya wananchi hawa wawapendao!

Tunaovinogozi wa dini wazuiao dhambi lakini huja wao wenyewe kushindwa kuishi bila hizo dhambi wazuiazo wewe usitende. Hapo huapata hoja za kulinda dhambi zao. Tutoapo sadaka twamtolea Mungu lakini matumizi ya sadaka atumia mchungaji na wenzake.

Tutamani jua wakati wa mawingu na mawingu wakati wa jua kali. Na labda huu ndio mfumo wenyewe wa maisha na labda ndio maisha yenyewe. Kweli maana mtoto anamtamani mzazi kuliko mtoto mwenzia. Mwanamume anamtamani mwanamke na mwanamke anamtamani mwanamume na ndio maana wawili hawa huaishi pamoja

Chama tawala huchukiwa zaidi na wananchi huku vyama vya upinzani vikipendwa kuliko vyama tawala na vyama hivyo pinzani hupenda kuingia madarakani kuliko wananchi
Labda ndio kanuni ya mvutana na msunguano. Misuguana ya vyuma huzalaisha umeme, huendesha mitambo nk na misuguana ya watu huzalisha ajira kwa wanasheria na hata jeshi huku misuguano wa mwili ikiliteleza mimba na kuzalisha watoto. Tuite nini hizi? Kanuni za maumbile?

Ila kuna visivyoendana. Tajiri hatamani kuwa masikini japo masikini wengi (sio wote) hutamani kuwa matajiri. Mwenye asiyechizi hatamani kuwa chizi. Anayetembea amevaa hatamani kutembea uchi labda chooni, bafuni na chumbani tu.

No comments: