Monday, October 15, 2012

nani mtoto kati ya mkojoleaji na mrusha mawe?

maisha yangu ya mwilli hayajawahi kuendelea bila kujiuliza na kuwauliza wengine kwa kujiuliza mimi mwenyewe

ndio, watoto wadogo katika udadisi wao na utoto wao wamekojelea kitabu cha dini, then watu wazima wenye akili timamu wakaja juu, wakarushiana mawe, wakarushia nyumba za ibada mawe na kuziharibu vibaya sana kutokana na watoto wadogo kudadisi fix za wazazi wao.

waafrika wengi tumelelewa kwa fix juu ya dini, vitabu vya dini na muumba. wanatwambia mara ukivitia moto haviungui, mara ukiviizarau huendelei mara usipoviweka chini ya mto unakolala utashambuliwa ma mashetani nk, yaani vimekuwa hiri vitabu hivi 

watu wamekuwa wakifanya majaribio mbali mbali ya hizi fix za vitabu vya dini (wenyewe huita vitakatifu), wengi huvilalia kwenye mtu, mimi niliwahi kulalia lakini sikuona chochote cha tofauti ni nikaacha!

sasa ilikuwa ni zamu ya dogo kule mbagala  kutest kkitu kingine, kwamba ukikojolea kitabu cha dini (na hii si kolani tu bali hata biblia kwa waitakayo iwe hivyo) utageuka nyoka, nguluwe au hagta kiumbe mwingine wa ajabu.

dogoa akatest zali, akafyatua kojo, utafiti wa dogo ukakamilika kuwa ni uongo, huwezi kuwa nyoka, paka wala kunguru kwa kukojolea kitabu cha dini, wala huwi chizi. katika elimu dogo kaelemika kuwa ni 'fix' takatifu hii!

watu wazima wenye akili timamu ya kuwalea wadogo wakaja una akili ndogo kilko za wadogo, wakarushiana mawe na kuharibu mali huko wakihumizana na kila mmoja akimshukuru Mungu kwa upuuzi huu, wakristo kwa waislamu wakashambuliana, kisa? dogo kawa mwanasayansi asiyepelekwa kibubusa (dogma)!!!!!

hii inatkana na fiks za viongozi wa dini badala ya kuwaambia watu ukweli. Mungu wetu wa dini ni wa mikwara, vitisho na kugeuza watu mijusi wakikojolea vitabu vyake, then hawageuki mijuis wana nini bali wanaendela kuwa watu wazima

jamani tuwe wakweli kwa watoto wetu juu ya Mungu mwenye kila uwezo na upendo na siofix wala adhabu. tuwe na busara na akili ya kuwelekeza wadogo na kuwapongeza wanapodhubutu na kugundua ukweli wao wenyewe

I remain

Kamala J Lutatinisibwa
jlkamala@yahoo.com
0754771601

Bukoba Rural Tanzania

2 comments:

Anonymous said...

asante kamala yaani sipati picha huyu dogo nimempenda ila majitu na mijaziba ya kipumbavu huyu dogo kakojolea karatasi yenye maandishitu yasiyokuwa na lolote na pindi haya maandishi yakitfsiriwa kwaswahili wote watajiona ni vichaambwa.sikumoja kwenye msikiti hapo Kimara jamaa kuna aya moja aliitfsiri kwakiswahili wale ambao hawajasoma wakasema kumbe ndio hivyo jamaa akasema eee!!!basi tangu sikuhiyo hata mimi moto ulizidi kupoa kwa mambo haya maana ulikuwa umeishapoa ila ulizidi kupoa zaidi.Halafu hata hii kwenda hijja huu ni utalii wa kidini lakini waarabu walivyokuwa wajanja wamelazimisha kuwa ni mojawapo ya nguzo ya kiislamu kumbe ni utalii tu maanampaka uende huko kwa mtu wa kutoka hapa tz lazima uwe na dola 4000=karibu millioni 8 sasahuoni kwamba waarabu wanatajirika lakini ukimwambia mtu aende pale Ndolage yanapoanguka maji anakwambia hapo ni mambo ya shetani wakati hatakule hakuna cha zaidi nikwenda kuona mambo ya kihistoria

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, sio Hijja tu ya Makka bali pia ile ya Israel kwa wakristo. wengi wanaamini haya ni mataifa ya kiMungu kuliko historia na ni kweli wanaingiza pesa nyingi sana kutokana na utumwa huu wa kiroho ulipo ktk jamii zetu