Wednesday, November 21, 2012

eti ni ya kweli haya malalamiko ya wanaume?

1. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake ni watu wa kulalamika, kukosoa
na wenye vijineno vya hapa na pale visivyo na maana na vyenye kukera.

2. Wanaume wanalalamika kwamba wanawake wanajaribu sana kuwadhibiti na
kuwakandamiza pale wanapoachiwa nafasi kidogo.

3. Wanaume wanadai kwamba wanawake huwa hawana furaha, mara nyingi
wanaonekana kama vile wako kwenye simanzi fulani na wanapenda sana
kununanuna hasa pale wanaume wanaposhindwa kuwatekelezea kile
walichotaka hata kama hakina umuhimu kwa wakati ule.

4. Wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanawanyima unyumba kama
adhabu ya kuwakomoa. Siyo kuwakomoa tu, bali huwa wanafanya hivyo kwa
lengo la kuwashurutisha wakubaliane na utashi wao fulani.

5. Lalamiko lingine la wanaume kuhusu wanawake ni lile la kwamba, huwa
hawafikirii kwa mantiki, bali mara nyingi kufikiri kwao huwa
kunakumbwa na mhemko. Kwa hiyo, uamuzi wao mwingi hauangalii mantiki
bali hujali zaidi hisia zao.

6. Wanawake wanalalamikiwa na wanaume kwamba, hali zao za kihisia huwa
hazitabiriki. Yaani huwa zinabadilika kufuatana na mabadiliko ya miili
yao ya kihomoni miilini mwao nyakati kama zile za siku zao(hedhi),
nyakati za ujauzito na hata wanapokoma kuziona siku zao(menopause) .

7. Wanaume wanawalalamikia wanawake kwa tabia yao ya umbea, kwamba
midomo yao huwasha sana hadi waseme kile walichokiona au kukisikia
hata kama si lazima na pengine ni hatari.

8. Wanawake wanalalamikiwa pia na wanaume kwamba, huwa wanatoka nje ya
ndoa, hasa wanapohisi kukosewa upendo ndani, jambo ambalo haliwezi
kuleta suluhu kwa tatizo hilo.

http://rosemarymizizi.blogspot.com/

No comments: