Wednesday, December 12, 2012

kuchanganya R na L kumeongezeka? anauliza mwanazuoni

utafiti wa bwana mmoja mhaya umebaini kuwa wahaya ni mabingwa wa makosa haya. yaani hata wale waliozaliwa mjini wanamakosa haya. kweli wengi wanakosea na labda inatia aibu, mimi kama mhaya nakubali kuwa wahaya wanaongoza na labda mimi ni mmoja wapo japo niko makini

fikiri jina langu eti ni Lutatinisibwa, kwa vyovyote iliaswa kuwa Rutatinisibwa. pia kwa kihaya, R na L zikichanganywa hazibadilishi maana ya neno kama ilivyo kiswahili au kiingereza. kwa mfano kula na Kura ni maneno mawili tofauti lakini Lutatinisibwa na Rutatinisibwa au mkulu na mkuru, maana ni moja tu.

tunaitaji utaalamu zaidi wa kiswahili


 Lutatinisibwa

No comments: