Sunday, January 27, 2013

"Ukitaka kumuona mkristo aliyechanganyikiwa, ni kwenye kujiuliza nani ni nani"Kuna mgogoro wa haki ya kuchinja kati ya mkristo na muislamu hapa nchini Tanzania. Viongozi wa kikristo wanadai nao wana haki ya kuchinja huku waislamu wakidai ya kuwa kwao kuchinja ni sehemu ya ibada! 

Bwana mmoja amesema kuwa ishara ya mkristo kuchanganyikiwa kwa kwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristo aka Nabii Issa, ni kwenye habari ya jino kwa jino au nani ni nani au kwenye kutafuta umaarufu wa kutafuta haki! Yesu Kristo aka Nabii Issa hakujishughulisha kabisa na habari za haki na akapiga marufuku habari ya jino kwa jino.
Kitabu maarufu kiitwacho biblia kinaonyesha jinsi jamaa walivyokuwa mahiri wa kuchinja mpaka kumtolea God sadaka ya damu kwenye agano la kale lakini hamna ushahidi juu ya kuchinja kwenye agano jipya ambalo ndilo mkamilisho wa agano la kale. Sioni Jesus akichinja au akielekeza wenzie kuchinja na nina wasi wasi kama huyu bwana alikuwa mla nyama au vegetarian

Labda hii ni habari ya humanity gone crazy, hivi mwmislamu akichinja, kile alichokichinja kinaacha kuwa nyama kwa mkrisito au mkristo akichini kile alichokichinja kinaacha kuwa Nyama kwa mwislamu? Hivi ni haki kweli kwa binadamu kuchinja na kutoa uhai ili ajishibishe kwa jina la dini?

Hawa jamaa sasa wanadai makundi kwenye machinjio ya kwamba yawepo machinjio ya wakristo na waislamu, je Makundi mengine wanayaweka wapi? Na je sisi tusiojishughulisha na biashara ya kuua na kula viumbe hawa wanatuweka wapi? Au na sisi nasi tuandamane kupinga habari ya kuchinja? (no hatuwezi kurudi tulikotoka -)
Sijiui kwa nini watu wahangaike na kuhakikisha dini zao zinapata lawama za kuuwa viumbe vingine kwa ajili ya kitoweo wakati sio lazima

Lutatinisibwa

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kwa nini kila mmoja achinje mwenyewe?

Anonymous said...

kamala wakristo wao wanakula mwiliwa yesu maana yy alijitoa kafara msalabani.halafu kitukingine mimi ndio maana naitaga kwamba huu ni ubangibangi,yaani watu wanalalamikia vitu vya ajabu kushindania kuchinja?yaani kweli waafrika tu wapumbavu