Saturday, February 16, 2013

Batamwa Rwamugila aachana na mwili wake!


Kuna mtu aliyekuwa akichangia sana kwenye blogs zetu hizi kwa njia ya anonymous na mara nyingine amekuwa akiacha jina lake kama Batwamwa Dar, ukweli ni kuwa sasa ameacha mwili au kwa lugha iliyozoeleka ya kushtusha amefariki dunia.

Batwamwa kafariki ijumaa 15/2/2013 katika hospital ya Muhimbili na atazikwa mkoani kagera juma lijalo. Ameacha mjane na watoto kadhaa

Huo ndio mwisho wake kama mwili japo anaweza ku re-incarnate,siwezi jua alivyoishi kama itakuwaje au atarudi kuzaliwa tena kama binadamu au viumbe vingine au kutokurudi katika dunia hii kwa njia yoyote. Nitajitahidi kushiriki maziko yake na labda kuwapeni taarifa zaid.
Lutatinisibwa

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimesoma habari hii kwa masikitiko makubwa sana...Batamwa nakumbuka jina hili kwa kweli na alikuwa hakusi kupita Maisha na Mafanikio kila siku na kuacha maoni..Jamani Mwenyezi Mungu na aipokee roho yake na apumzike kwa amani peponi.poleni sana wafiwa huu ni msiba wa wote kwa kweli..Kamala tuwakilishie na sisi. Siss tulimpempenda ila Mungu kampenda zaidi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

karibu sana Yasinta. mwmisho wa kutoa rambirambi ni tarehe 1/3 so karibu sana