Wednesday, February 13, 2013

maoni ya Padri P Karugendo juu ya Kujiuzulu kwa PaPa

Bubelwa Kaiza,
Asante sana kwa ujumbe wako. Binafsi sikushangaa kwa Papa huyu kuachia ngazi. Huyu ni mtu ninayemfahamu kwa karibu. Ni mwanamapinduzi ambaye amekuwa akizimwa kwa kuchaguliwa kuchukua nafazi nzito katika kanisa.
 
Huyu ndiye aliyewafundisha wanateolojia wa Latin Amerika, ambao waligeuka kuwa mwiba wa kanisa; ili kuzima moto huo Ratzinger, alichaguliwa kuwa mlinzi wa imani ya  kanisa katoliki. Na yeye akawa ni hakimu wa kuwachinja wanafunzi wake! Alipochaguliwa kuwa Papa, alitangaza msamaha kwa wanafunzi wake wa Latin Amerika. Sina uhakika kama mapadri hao walirudi kanisani.
 
Kumpatia Upapa, iliku ni hatua ya kumzima zaidi, maana alitaka kuachia ngazi ya ulinzi wa  imani, kabla ya kifo ch Papa John Paul 11, ili aandike vitabu. Alikataliwa, akaombwa aendelee na baada ya kifo cha Papa John Paul 11, akateuliwa kuwa Papa.
 
Hata hivyo aliendelea kuandika. Na kama mnakumbuka kitabu chake cha mwisho ni Yesu wa Nazareti na hoja kwamba miaka inayotajwa kwenye biblia ya kuzaliwa kwa Yesu, ni uongo. Na akaenda mbali kuruhusu matumizi ya kondomu kwa wanandoa ambao mmoja wao ana virusi. Ukisoma kitabu hicho chaYesu wa Nazareti, utagundua kwamba mtu ambaye kanisa lilikuwa na nia ya kuzima mawazo yake kwa kumpatia madaraka ya juu, alianza kuvunja kuta na kutaka kuwa huru.
 
Kanisa Katolili ni taasisi na lina wenyewe ambao kwa kiasi kikubwa hawataki mambo yabadilike.
Hivyo inawezekana kabisa, Papa Benedicto, ameshinikizwa kuachia ngazi baada ya kugundua kwamba hawawezi kumzima na nafasi yake ni kubwa kwa kuweza kufanya chochote na akasikilizwa.
 
Lakini pia, kufuatana na uanamapinduzi wake,inawezekana kaamua kuachia ngazi mwenyewe. Hayo ndiyo maaoni yangu juu ya Papa kuachia ngazi. Historia itatueleza siku ikifika.
Na Kanisa katoliki, lilivyo anaweza kufa hata bila kufikia tarehe hiyo iliyotajwa! Na yeye kwa kulijua hilo hakumshirikisha mtu yeyote juu ya uamuzi wake. Wangejua mapema, wangemmalizia kabla ya kutangaza hatua yake hiyo!
Padri Privatus Karugendo.

No comments: