Wednesday, September 18, 2013

Mavumbini ulitoka, kwenye sement na zege utarudiTangu mwaka jana mwezi wa nane mpaka septemba hii nimezika wapendwa watatu.  kwa misiba ya kikristo tumezoea kuona viongozi wa dini wakizika kwa kuwaambia waliokufa ya kuwa mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi. Kwa uzoefu wa misiba hii ya kisasa, kauli hizi haina mashiko tena na zinastahili kuboreshwa

Katika misiba ya jamaa zangu ya hivi karibuni sikushuhudia hata mwili mmoja uliozikwa mavumbini bali kwenye sement, vigae mpaka zege. Sijui ni kwa nini binadamu tumeiga mfumo huu wa kazikana kwenye ma septic tanks.  Sijui ikitokea kijitundu kwenye kaburi na maji ya mvua yakajaa kaburiki itakuwaje mabaki ya mfu au  wezi wakija kuchukua nondo zao kaburi likabaki wazi

Makaburi ya siku hizi haswa kwa wenye nazo yanajengwa na kuwekewa naksh mbali mbali na mengine yanaboreshwa kila uchao. Kwenye kuzika sasa, watu hawajazi tena maundogo shimoni bali hurusha vijimaua kiasi juu ya majeneza yalotengezwa na kunakishiwa kinoma kabala ya kufungwa kwa zege iliyoshindiliwa siment kali na hivyo kuzuia uwezekano wowote wa mwili wa marehemu kuguswa na kiiudongo chochote.

Je sio wakati muafaka sasa kwa viongozi wa dini kuacha kusema  mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi badala yake wasema Mavumbii ulitoka, kwenye sement na zege utarudi?

No comments: