Friday, September 13, 2013

visa na mikasa ya wahamihaji haramu KAGERA

misako mikali inaendelea mkoani kagera, magari ya polisi yaliyosheheni
FFU, JWTZ na mofisa waliovalia kiraia (UWT, PCCB etc) yanaonekana
yakikimbia kama vile yanaendeshwa na vichaa wasiojali uhai wao.

hufika mahala wengine wakasombwa kibahati mbaya. nikiwa maeneo ya
ibwera, nakutana na jamaa mwenye asili ya Rwanda, hali halali,
anasimama milimani akiona gari la binafsi linakuja nduki anakimbilia
porini na kujificha pangoni

jamaa huyu amezaliwa hapa miaka ya sabini, babayake na mama
walimtelekeza na kurudi rwanda na hana mawasiliano nao tangu 1994.

ila sasa imengia siasa pia, nimekutana na bwana mmoja anapanga
kugombea udiwani uchaguzi mkuu ujao, huyu bwana anataka kuchuana
kwenye kata ya meya wa sasa, kapelekeshwa, anasema amelala Lupango ya
uhamiaji kwa siku 7 bila kupelekwa mahakamani, akawa mbogo na
kwalazimisha wampeleke mahakamani

ndo kaachiwa kwa sharti kuwa ajaze mafuta kwenye gari la
polisi/usalama, then awapeleke maofisa kijijini kwao izimbya na
kuwaonyesha makaburi matano ya babu zake ili kuuthibitisha uraia wake!

inasemekana hawa jamaa wakikutilia shaka wanataka vitambulisho,
usipokuwa navyo unaammbiwa imba wimbo wa taifa, ikishindikana basi
imba ile tanzania tanzania nakupenda.........

raia wenye asili za kigeni wote hapa matumbo yao ni ya moto hapa na
wengine wanatamani kuhama mkoa. swali kujiuliza ni je, kwa nini watu
kutoka rwanda, burundi, Uganda etc wanapenda kukimbilia na kujichimbia
hapa nchini lakni hawaombi uraia wala kuwa na nyaraka halali kwe wengi
wao?

No comments: