Wednesday, March 5, 2014

Kazaura alikutana na wasomi wa kabila lake maeneo tofuauti ya ulayaKatika mazishi ya aliyekuwa mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, mwenyikiti wa Bodi ya shirika la umeme nchini Tanesco, naibu katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki, balozi mstaafu na vyeo vingine lukikuki yalijitokeza mambo kadha wa kadha. Kubwa zaidi kuliko yote ni ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  mazishi hayo.

Katika kitongoiji cha Kateiganilo kijijicha Igurugati kata ya Bugandika mkoani Kagera ndipo mazishi ya balozi Kazaura yalifanyika jumamosi ya Tarehe mosi Mwezi machi mwaka huu. Zilikuwa ni ibada baada ya ibada na ibada ya mazishi ilichukua muda mrefu kwakweli ikiongozwa na askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera Mhashamu Methodius Kilaini. 

Mazishi hayo yalithibitisha ni kwa kiasi gani serikali ikiamua mambo yanaweza kuwa mazuri. Ilijengwa bara bara nzuri sana ya changarawe kuelekea Nyumbani kwa Marehemu ambayo haijawahi kushuhudiwa mahali pale tangu uwepo wa kijiji hicho, huku Umeme ukiwaka bila hata kucheza kama ilivyozeleka.

Ujio wa raisi haukuwa jambo la kawaida kijijini Igurugati kwani watu walihamaki kumuona, huku baadhi ya wazee wakijadili ukaribu aliokuwa nao Balozi Kazaura kwa Rais Kikwete na wengine kwenda mbali na kusema kuwa Bugandika imebarikia sana kwa Kikwete (wengi hutamka Kikweete) kuikanyaga ardhi yao ya Bugandika.

Pamoja na kwamba kata Bugandika imezalisha wasomi wengi na watu mbali mbali, bado ni kata ambayo iko nyuma kielimu. Shule waliosomea akina Balozi kazaura na wengine haivutii kuingalia machoni. Zahanati nayo haina umeme wala wodi ya kulaza akina mama. Sijui wagonjwa na wazazi wanaokimbbilia pale usiku inakuwaje huduma yao

kubwa zaidi ni labda marehemu Kazaura hakuwahi kuchunga mifugo, kuchanja kuni au hata kuchota maji. Hii inatokana na wale wote walioongea juu ya walivyomfahamu marehemu kuwa na uzoefu wake katika anga za kimataifa zaidi. Wengi wa walioogelea jinsi wallivyomfahamu Balozi kazaura ni maprofesa na Madokta mbali mbali.  Majina kama Profesa Rweyemamu, Mutasa, Kagaruki nk yalisikika.
Wote hawa hakuna aliyewahi kukutana na marehemu mitaani ila walikutana naye zaidi ulaya na marekani katika mikutano mbali mbali na masomo yajuu. Nilisikia mtu mmoja tu aliyeongelea habari za kusoma naye shule ya Ihungo iliyoko mmkoani Kagera. Hizi ndo huwa swaga za  Kagera bwana, Shumaalamu waitu

No comments: