Monday, March 9, 2015

Dini, Azaki, vyuo au wanasiasa wa kuikomboa tanzania?

Dada Anna,

umetoa mchango mzuri juu ya nafasi ya Dini na taasisi zake kushirikikuleta mabadiliko chanya na katika mchango wako huo ukiangalia kilamchhangiaji anaukwepa, hakuna anayetaka kuona nafasi ya dini katikakuikomboa jamii yetu na ukigusa dini kila mtu anacharuka na kuanzakuiteetea utafikiri dini zetu na viongozi wake wanaisi mbinguni na sioduniani.


upande wa TZ, dini ziko upande wa wakandamizaji na naweza kusema yakuwa dini zetu zinasapoti mafisadi, wezi wa kisiasa na CCM maslahi.nyakati za kampeni viongozi wa dini hizi huja na kauli za kutukuzautawala kama vile Kikwete ni chagua la Mungu-Kilaini na Kulola,kikwete ni kama mfalme daudu-Malasusa


then viongozi hawa wanatwambia kuwa mamlaka zote hutoka kwa Mungu. nabaada ya hapo, wanasiasa wenye utajiri ndio hushiriki kwenye harambeeza kidini na huwa na nafasi maalumu kwenye Nyumba zetu ibada.hhuchangia hela Nyingi na haki ya Mungu hamna kiongozi wa dinianayeweza kusimama na kukemea wizi wa wanasiasa, uliwahi kumsikiakiongozi wa dini ipi akikemea wizi na ufisadi na kukataa michango yamafisadi kuwa inanuka rushwa?


viongozi wachache wa dini wanaojaribu kuwa upande wa wanachiwanathibitiwa kwa kuwa ni wasaliti kama ilivyo kwenye vyama vya siasa.kwa mfano padre Kalugendo alijipambuanua na maambukizi ya VVU kwawaumini kwa kuwaambia kuwa watumie Kondomu kinyume na mafundisho yakanisa. Karugendo alifukuzwa upadre kwa usaliti japo baadae kanisakatoliki lilikuja kukubaliana na mitizamo ya kikarugendo kwa kutambuamatumizi ya kondomu kwa wanandoa! na usaliti wa karugendo haujaisha nakumrudisha U-padreni


kwa hiyo dada Anna, unapoipigania jamii ya KiTZ ujue tunapaswa kuepukaviongozi wa dini hizi.


neno usaliti katika vyama vya siasa linatumika kukamilisha maslahi yawanasiasa wanaovingoza.


vyame vyetu vikubwa vya CCM, CUF, Chadema, NCCR, TLP, nk vimekuwavikiita baadhi ya viongozi wao kuwa ni wasaiti na kuwafukuzauanachama. kwa kifupi ni kwamba vama vyetu haviwezi kuamini katikakukubaliana katika kutokukubaliana na maisha ya kaenda, ni lazimammoja 'afe' ili mwingine aweze kutawala vizuri. mpaka jamii yetuikiweza kufikia hatua hiyo ndipo tutakuwa na vyama imara vinavyowezakuleta mabadiliko halisi


hata sisi watanzania tukiweza kuongozwa kwa itikadi na imani thabiti.utaona watu wanahaha kutoka chama kimoja kwenye kingini kwa kauli zakijinga mara nimerudi nyumbani, mara chama hiki hakifai nk, na ndiomaana waTZ wa vijijini hushindwa kujua wafuate itikadi ipi.


ni kwa nini bila kujali kuwa kuna UKAWA, CCM wala chadema, asasi zakiraia, watu binafsi wasiokuwa wana asasi wala wafuasi wa vyama,taasisi za kidini kwa ujumla wake, Vyuo na hata vyombo vya habarivisikae pamoja na kuteua watu wanaostahiri kutuongoza na kuwaomba auhata kuwalazimisha kugombea nafasi stahiri na kuwaambia wanaachi kuwamtu faluni ndiye anayepaswa kuongoza Taifa hili bila kujali chamachake, dini yake wala ubini wake na kumpigia kampeni?


ni kwa nini Taasisi hizi ziko kimya na kuliacha jukumu hili kwa vyamava siasa pekee then baadae vinakuja kusifia na kukosoa matendo yaowakiishakaa madarakani, kuchukua fedha zao kwa njia ya Sadaka namichango huku tukilaghaiwa kuwa viongozi wote hutoka kwa Mungu hukutukijua awagombea wetu ni wezi, mafisadi na watendo maovu kibao dhidiya ubinadamu?


tukifikia hatua ya kuw ana Mgombea binafsi/pekee angalau itaimarishavyama kwani vitajua zairi shairi ya kuwa vikimmtimua tu mtu atasimamayeye kama yeye kugombea na sio Chama.
Dada Anna mfano wako ulioutoa wa mwanaharakati na mwanachama kwendakutuo semina kwa chama kingine moja kwa moja kwa mfumo wetu ni'usaliti'. ni bora ukawasaliti wapiga kura wako kuliko chama, maanachama hakitakufukuza wala kukusema.


mabadiliko halisi kwa watanzania haawezi kuletwa na taasisi hizitulizonazo za kidini, Asasi za kiraia wala vyama vyya siasa,tunahitaji kizazi kipya kissichoangalia sana taasisi hizi barakinachoona uhalisia na kupigania haki ya watanzania wote

No comments: